Jukwaa la Mazungumzo la Tehran lilifanyika jana Jumapili, Mei 18, kwa kuhudhuriwa na Rais Masoud Pezeshkian, Waziri wa Mambo ya Nje, Abbas Araghchi na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje kwenye Kituo cha Mafunzo ya Kisiasa cha Wizara ya Mambo ya Nje.
Sayyid Abbas Araghchi amewaambia waandishi wa habari waliokuwepo katika mkutano huo kwamba: "Muda wa mazungumzo hayo umeshapangwa na utatangazwa hivi karibuni."
Akijibu swali la iwapo Tehran imepokea ujumbe wowote wa maandishi kutoka Oman na Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Hatujapokea ujumbe wowote wa maandishi kutoka Oman. Duru ijayo ya mazungumzo baina yetu na Marekani huenda ikafanyika hivi karibuni, na wakati na mahali vitatangazwa hivi karibuni."
Kuhusu mkutano wa pande tatu kati ya Iran na nchi za Qatar na Oman, Sayyid Abbas Araghchi amesema: "Mazungumzo yalikuwa mazuri sana. Tulijadiliana matukio ya hivi karibuni na masuala ya kikanda, mahusiano baina yetu na nchi hizo mbili, na mazungumzo yanayoendelea kati yetu na Marekani."
Hadi hivi sasa Iran na Marekani zimeshafanya duru nne za mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana kwa upatanishi wa Oman. Ajenda kuu za mazungumzo hayo ni kadhia ya nyuklia na kuondolewa vikwazo Iran.
342/
Your Comment